In Creative Corner, poetry

Kaniaga kaondoka, kaamba huku hafai,
Motoni pana mashaka, peponi ndipo tamrai,
Mechoshwa na wahaka, kule yeye tafurai,
Kaibwaga etu mila, mesafiri utumwani.

Maskani masikini, ulaya tapata mali,
Mekana utamaduni, mekita tangu azali,
Maisha nyuma ni duni, kule mejawa asali,
Kaibwaga etu mila, mesafiri utumwani.

Lipofika alimaka, katengwa kisa rangi,
Kabadili yake hulka, mjini kawa shangingi,
Kabakia hana kaka, mtumwa wa shilingi,
Kaibwaga etu mila, mesafiri utumwani.

Lebasi kawa bikini, danguro kwake makazi,
Kahisi yu mbinguni, kafumba yake maozi,
Hivi yeye kauleni, kawasaliti wazazi,
Kaibwaga etu mila, mesafiri utumwani.

Lugha yake mebadili, ya kwetu haimanyi,
Nyuma tena astahili, maisha hayabambanyi,
Tamaa memtia aili, bingwa yeye humkanyi,
Kaibwaga etu mila, mesafiri utumwani.

Huko yeye zumbukuku, kahisi yuko jelani,
Sasa mejawa shauku, mlo kwake jalalani,
Meshajawa dukuduku, jakamoyo mtimani,
Kaibwaga etu mila, mesafiri utumwani.

 

 


This poem was published in the 9th Issue of PoeticAfrica magazine.
Please click here to download.

More Poems:

Nashangaa – Raymond Mpalile (Tanzania)
Soliloque par Mayssa Boulmaali (Algérie)
Journey to my Dream – Shifaa Ibuni (Tanzania)

 

Recommended Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt

Kaibwaga Etu Mila na Kimani Halima (Kenya)

Time to read: 1 min
0
Soliloque par Mayssa Boulmaali (Algérie)Funminiyi Akinrinade